Daniela msichana anayeteseka na penzi la Migual:
Daniela msichana ambaye ni rafiki wa Ana Paula ambaye pia wamesoma nae chuo kimoja cha uuguzi,mwenye mapenzi ya dhati na kijana Migual kaka yake na Ana Paula mapenzi ambayo yanampa wakati mgumu sana kutokana na mpenzi wake huyo (Migual) kuwa mwanaume asiyekuwa na msimamo wa kimaisha kutokana na upeo wake wa kimawazo kuwa mdogo hali inayopelekea kumpa majaribu dada yake Ana Paula kwa matukio yake mabaya ya kila mara.
Kitu ambacho pia kina mponza zaidi Migual ni Ulevi ambao hauna maana ambao umekuwa ukimletea matatizo kila kukicha na kufanya maisha yake kuwa kama mzigo kwa Ana Paula lakini pamoja na matatizo hayo mengi kwa dada yake huyo,Ana Paula amekuwa bado ni msaada mkubwa sana kwa kaka yake huyo ambaye ndiye aliyesababisha kwa kiasi kikubwa Ana Paula kusain mkataba wa ndoa na Rogelio
Lakini pamoja na misuko suko aliyonayo kijana Migual bado mwanaume katili Bruno anaamua kutumia mwanya wa matatizo yake Migual na kumtumia katika mambo yake mengi ikiwemo na kupata siri za maisha yao ya nyuma kabla ya Ana Paula hajaolewa na Rogelio kutokana na udhaifu wa akili ya Migual ,Bruno anakuwa anapata nafasi ya kupata mambo mengi ya siri kwa Migual mara baada ya kumlewesha .
Daniela akiwa kama mwanamke mwenye msimamo na Mapenzi yake kwa Migual kwani ni mara nyingi amejikuta katika matatizo makubwa hii ni kutokana tu na kujulikana ni mpenzi wa Migual pamoja na matizo mengine ni pamoja na kwenda jela mara kwa mara ili kumuangalia mpenzi wake huyo (MIgual) pale anapokuwa ameswekwa jela lakini pia Migual anakua akitengana tengana na mpenzi wake huyo(Daniela) kwa kisingizio kwamba hawezi kuwa na furaha kwake .
Lakini kwa misuko yote kwa sasa penzi limerudia tena kwa kasi ya ajabu hii ni baada ya Migual kugundua kutokana na mapungufu aliyonayo hakuna mwanamke atakaye mpenda kwa Dhati kama ampendavyo sasa Daniela