Jumanne, 31 Desemba 2013

Daniela msichana anayeteseka na penzi la Migual:
Daniela msichana ambaye ni rafiki wa Ana Paula  ambaye pia wamesoma nae chuo kimoja cha uuguzi,mwenye mapenzi ya dhati na kijana Migual kaka yake na Ana Paula  mapenzi ambayo yanampa wakati mgumu sana kutokana na mpenzi wake huyo (Migual) kuwa mwanaume asiyekuwa na msimamo wa kimaisha kutokana na upeo wake wa kimawazo kuwa mdogo hali inayopelekea kumpa majaribu dada yake Ana Paula kwa matukio yake  mabaya ya kila mara.
Kitu ambacho pia  kina mponza zaidi Migual ni Ulevi ambao hauna maana ambao umekuwa ukimletea matatizo kila kukicha na kufanya maisha yake kuwa kama mzigo kwa Ana Paula lakini  pamoja na matatizo hayo mengi kwa dada yake huyo,Ana Paula amekuwa bado ni msaada mkubwa sana kwa kaka yake huyo ambaye ndiye aliyesababisha kwa kiasi kikubwa Ana Paula kusain mkataba wa ndoa na Rogelio
Lakini pamoja na misuko suko aliyonayo kijana Migual bado mwanaume katili Bruno anaamua kutumia mwanya wa matatizo yake Migual na kumtumia katika mambo yake mengi ikiwemo na kupata siri za maisha yao ya nyuma  kabla ya Ana Paula hajaolewa na Rogelio kutokana na udhaifu wa akili ya Migual ,Bruno anakuwa anapata nafasi ya kupata mambo mengi ya siri kwa Migual mara baada ya kumlewesha .
Daniela akiwa kama mwanamke mwenye msimamo na Mapenzi yake kwa Migual kwani  ni mara nyingi amejikuta katika matatizo makubwa hii ni kutokana tu na kujulikana ni mpenzi wa Migual  pamoja na matizo mengine ni pamoja na kwenda jela mara kwa mara ili kumuangalia mpenzi wake huyo  (MIgual) pale anapokuwa ameswekwa jela lakini pia Migual anakua akitengana tengana na mpenzi wake huyo(Daniela) kwa kisingizio kwamba hawezi kuwa na furaha kwake .
Lakini kwa misuko yote kwa sasa penzi limerudia tena kwa kasi ya ajabu hii ni baada ya Migual kugundua kutokana na mapungufu aliyonayo hakuna mwanamke atakaye mpenda kwa Dhati kama ampendavyo sasa Daniela

happy new year 2014

Jumatatu, 16 Desemba 2013

baby fashion

hadi rahaa






Je wajua kuwa Celyn na liam ni wapenzi kweli kwel?
 Kim chiu au (Celyn) kaa tulivyomzoea na kama ambavyo amejipatia umaarufu katika tamthilia ya ina kapatid anak  au(  her mother's daughter) ni binti mdogo mwenye  umri wa miaka 23 tu ,kwani amezaliwa mnamo mwaka 1990 mwezi april tarehe 23 amejizolea umaarufu mkubwa sana baada ya kuanza kuigiza filamu za vichekesho 2011 ambayo iliitwa My Binondo Girl ambayo ilimpa umaarufu sana na akiwemo pia mpenzi wake Xian lim ambae kwa sasa anajulikana kama liam kwemye tamthilia hii ya (her mother's daughter)ambayo wameigiza kama marafiki wanao gombana ovyo kila wakionana





 Celyn akiwa na mpenzi wake liam
Kama ilivyo sasa kwenye tamthilia ceyln si msemaji wa matatizo yake na ndo ilivyo kwenye maisha yake Celyn pia si msemaji wa shida zake zinazo msibu kwa watu  na vitu anavyovipendelea celyn ni pamoja na kusafiri ,mitindo, na michezo pia tamthilia hii ya her mother's daughter inafanya vizuri sana ulimwenguni na imempatia tuzo ya Philippine's Yahoo OMG! awards, 2013
Pia Celyn  hajaanza kuigiza leo na wala hii siyo Tamthilia yake ya kwanza kuonekana ameshaigiza thamthilia nyingi na kutumia majina mengi tofauti tofauti hivyo hata siku ndugu msomaji utakapo bahatika kwenda philipino na kukutana na binti huyu mrembo hutotumia jina la celyn kama tulivyo zoea kwani ana majina meeengi sana kutokana na tamthilia hizo nyingi kuigiza  
Baadhi ya kazi ambazo amewahi kuzifanya na majina ambayo amewahi kutumia
 My Fairy Kasambahay  akijiita Elyza      hii tuijuayo sisi ambayo ameigiza mwaka  2012-2013 Ina, Kapatid, Anak ametumia jina la  Celyn Marasigan-Lagdameo mwaka  2012 aliigiza tamthilia iitwayo  Maalaala Mo Kaya: Kalendaryo  akitumia jina la Pauline Chaves  mwaka 2011-2012  akiigiza nyingine iitwayo My Binondo Girl Jade

Ijumaa, 30 Agosti 2013

                                                   lazima tuwatafsirie
                                                        yes hapa ndo kwao
hivi karibuni kwenye HAPA NDO KWAO